Wakati mwingine napenda sana kuzikiliza maishairi ya mrisho Mpoto. Lakini mwisho wa mwaka jana nilikuwa nae laivu na kupata maneno yake matamu. moja ni kuhusu sisi waafrika kuwashobokea sana wazungu na lingine ni swala la brain drain. hitimisho la maneno yake lilikuwa kama sisi waafrika tunataka kuendelea basi hatuna budi kufanya kazi kwa bidii, uaminifu na kwa kutumia busara ilikiwa ni pamoja na kulinda rasilimali za nchi kama vile madini, wanyama pori lakini pia kuhakikisha rasilimali hizi zinawanufahisha watannzania wote bila kujali kabila, rangi, kipato, mrengo wa siasa na mengine mengi yanayoweza kuwatenganisha watu
No comments:
Post a Comment