Pages

Tuesday, September 14, 2010

Uzinduzi wa Tamko la Wanaharakati wasio wa Kiserikali kuelekea na baada ya Uchaguzi Mkuu 2010 na Mdahalo

wadau hii ni fursa nzuri kwako kama mpiga kura kushiriki na pia kama mtanzania anayejali nchi yake
Ndugu,






Asasi ya Agenda Participation 2000 (AP2000) inapenda kukulika katika uzinduzi wa Tamko la Wanaharakati Wasio wa Kiserikali 2010, Wakati na Baada ya Uchaguzi 2010: Tanzania Ipi Tunayoitaka? (Non-State Actors Charter 2010) na kuhudhuria mdahalo wenye mada kuu ya; "Tanzania Ipi Tunayoitaka sasa na baada ya Uchaguzi Mkuu 2010".





Tamko hili la Wanaharakati Wasio wa Kiserikali ni matokeo ya juhudi za kuunganisha asasi za kiraia zaidi ya 150 zilizokuwa zimeanza mnamo mwaka 2005. Tamko hili linawasilisha mijadala, mapendekezo kwenye maeneo muhimu ambayo wananchi wangependa yashughulikiwe sasa na hata baada ya Uchaguzi Mkuu 2010.





Shughuli hii ya uzinduzi itafanyika siku ya Jumanne, Septemba 21, 2010 katika Hoteli ya Blue Pearl, Ubungo Plaza kuanzia saa mbili unusu asubuhi hadi saa nane mchana.





Wanasiasa wanaongea, wagombea wanaahidi. Njoo ujiunge nasi kama wananchi tupaze sauti zetu zisikike katika mustakabali wa Taifa letu la Tanzania tunalolitaka sasa na baada ya Uchaguzi Mkuu 2010. Tumeambatanisha rasimu ya ratiba ya siku ya uzinduzi.





Muhimu: Kwa watakaopenda kuhudhuria uzinduzi huu na mdahalo, tafadhali wathibitishe kuhudhuria kwao kupitia barua pepe; dalali@corruptiontracker.or.tz au simu: 0717-011112 au 0758-318914.





Wenu,

Michael J. Dalali

Afisa Programu,

Agenda Participation 2000.

No comments: