Pages

Wednesday, March 16, 2011

Rostam aponda tiba ya Mchungaji Loliondo

Tuesday, 15 March 2011 21:22

0diggs

digg

Shija Felician, Igunga

WAKATI Watanzania wengi wakimiminika kwenda wilayani Loliondo, mkoani Arusha kupata dawa inayodaiwa kutibu magonjwa sugu, Mbunge wa Igunga (CCM), Rostam Aziz ameibuka na kusema tiba hiyo haina lolote akidai kwamba ndugu zake watano wameitumia lakini hawajapona.Akihutubia wananchi katika mkutano wa hadhara wa kuwashukuru wapigakura uliofanyika kwenye Viwanja vya CCM wilayani Igunga, Tabora mbunge huyo alisema haiamini dawa hiyo kwa kuwa ana ushahidi kwa ndugu zake hao ambao anadai kwamba wanaendelea kuugua kisukari licha ya kutumia dawa hiyo siku saba zilizopita.Aliwataka wale watakaokwenda Loliondo ambao wanatumia dawa za hospitalini kuendelea kuzitumia badala ya kuzipuuza na kuzitupa... “Ndugu zangu wananchi wa Igunga, mimi mjomba wangu Hassan mnamfahamu karibu wote hapa mjini ni mgonjwa wa siku nyingi wa kisukari. Ameshakunywa dawa hiyo lakini mpaka sasa ni mgonjwa kama mnavyomuona sasa hiyo dawa inaponyesha nani?”Hata hivyo, aliwataka wananchi wote wenye imani juu ya dawa hiyo waende huku akiwasisitizia kutopuuza ushauri wa madaktari kwani.Wakati Rostam akipinga dawa hiyo, wilayani Kahama, mamia ya wafanyabiashara wamefunga shughuli zao na kukimbilia Loliondo kwa Mchungaji Mwasapile kunywa dawa hiyo huku baadhi ya waliorejea baada ya kuinywa wakidai kuwa hali zao sasa ni nzuri.Wafanyabiashara hao wengi wao wanaondoka kwa siri wakidai wanakwenda Dar es Salaam katika shughuli zao, lakini siri imefichuka baada ya baadhi yao kuoneka katika runinga wakiwa katika foleni wakisubiri kupatiwa huduma hiyo.Mbali ya kuzungumzia suala hilo la tiba ambalo limegusa hisia za wananchi wengi wa Afrika Mashariki, mbunge huyo aliwapa pole wananchi wa Igunga ambao nyumba zao zimeezuliwa na upepo uliosababishwa na mvua kubwa zilizonyesha wiki iliyopita ambazo ziliathiri kaya 19. Aitoa msaada wa Sh500,000 kwa kila kaya iliyokumbwa na maafa hayo.

Add this page to your favorite Social Bookmarking websites

No comments: