Pages

Friday, July 25, 2014

Matokeo ya kidato cha nne na changamoto zake

Unajua maana ya BIG RESULTS NOW?? Fuatilia matokeo haya ya kidato cha sita.

Division zero mwaka jana 2604, mwaka huu 612. Tofauti watu 1992, sawa na asilimia 325%.

Division one, mwaka jana 325, mwaka huu 4,365. Tofauti 4040, sawa na asilimia 1243%. Haya ni maajabu ya karne.

Walitanua ukubwa wa goli ili iwe rahisi kufunga... Kutoka zero zaidi ya 2000 mwaka jana hadi zero 600 tu mwaka huu. Kutoka div.one 300 tu mwaka jana hadi one zaidi ya 4,000 mwaka huu.

Hivi waalimu walewale wa shule zilezile zilizotoa one 300 mwaka jana ndo wametoa one 4,000 mwaka huu??

Changamoto zao zimetatuliwa? Maabara zimejengwa? Vitabu vimeongezwa? Madai ya walimu yamelipwa? Waalimu wa Kiswahili wameacha kufundisha Hesabu kutokana na ukosefu wa waalimu wa hesabu?

Kama changamoto hizo zote hazijatatuliwa mabadiliko haya ya ghafla kutoka div.one 300 hadi div.one zaidi ya 4,000 yametoka wapi? Kweli tumeamua kutanua goli tufunge kirahisi. Karibu Tanzania, hii ndiyo BRN bhana.!

Wanasema BRN means Big Results Now, mimi namwambia Waziri Kawambwa BRN, yani he should "Better Resign Now" maana watoto wetu wanapata BRN = Brain Receive Nothing.!!

Haya tia neno

No comments: