Wadau,
Staki kuthibitisha haya maneno hapo chini kama ni kweli au si kweli,
kwani kipindi hiki mambo mengi yanajitokeza.
Kinachonisikitisha naamini usajili tuliofanyiwa wa simu zetu ulikuwa
ni uhuni mkubwa, kwani sasa hivi unaweza ukapata ujumbe hususan toka
CCM (nasikia hata CHADEMA), ukikuomba kuchangia au kueleza mafanikio
ya CCM, kitu kinacholeta picha kuwa namba zetu zinatumika kisiasa
bila ridhaa yetu.
"Kila Mtanzania anayepiga simu mtandao wowote, asilimia kumi (10%) ya
huo muda wa maongezi, fedha hizo zinaenda kuchangia Kampeni za CCM.
Kudhihirisha hili, mtu yeyote mwenye simu, chukua simu yako, nenda
kwenye sehumu ya kuandika ujumbe mfupi (SMS); kisha andika neno
"HAPANA" na tuma ujumbe huo kwenda namba "15016." Utapokea ujumbe huu
“Asante kwa ujumbe wako, utatolewa kwenye huduma hii ya changia
ushinde na CCM.”Hii ni hujuma tunayofanyiwa watumiaji wa huduma za
mawasiliano bila ridhaa yetu au kujulishwa hivyo na Mamlaka ya
Mawasiliano Tanzania (TCRA).
Kesho yake, October 14,2010, nadhani baada ya wahusika kushtukia idadi
ya watu watu wanaojiondoa kwenye huduma hii; na nilipokuwa najiondoa
kwenye hujuma hii kwa kutumia lini yangu ya Zain & Zantel, nilipokea
ujumbe huu “Asante kwa ujembe wako kama umeshiriki Changia ushinde
utaondolewa kwenye huduma. Kumbuka hakuna malipo kutumia mtandao wa
mawasiliano wa CCM.” Ujumbe huu wa pili nauona kama ujanja wa
kuwapumbaza watu kwani mantiki yake imevurugwa kwa maksudi. Hata hivyo
cha msingi hapa tusiangalie nyuma, tumeshahujumiwa, dawa ni kujiondoa
maana kujiondoa kwenye hujuma hii ni bure. Mjulishe ndugu na rafiki
yako tafadhali. "
Noel
No comments:
Post a Comment