Pages

Tuesday, October 19, 2010

UFAFANUZI KUHUSU FURSA KWA WANAFUNZI KUPIGA KURA CHUONI WAKATI WA LIKIZO

Hiki ninaona kama kiini macho kwani mwanafunzi aliyeko kigoma atakuja kwa gharama ya nani? wadau hii imekaaje. wanaharakati tupambane kuhakikisha wanafunzi wanapiga kura. this might be a strategy for CCM to ensure that majority of University students who are tied with ccm are not going to vote.


CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM




UFAFANUZI KUHUSU FURSA KWA WANAFUNZI KUPIGA KURA CHUONI WAKATI WA LIKIZO

Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kinapenda kufafanua kwamba, ingawa tangu tarehe 24 Julai mwaka huu wanachuo walio wengi wamekuwa mapumzikoni, hakuna kampasi yoyotote ya Chuo Kikuu iliyofungwa. Shughuli zote muhimu za Chuo, zikiwemo ufundishaji wa makundi kadhaa ya wanafunzi wa shahada za kwanza, utafiti, huduma za maktaba, utoaji wa ushauri wa kitaaluma na shughuli mbalimbali zinazohusiana na mafunzo ya uzamili na uzamivu zimekuwa zikiendelea muda wote. Kwa kifupi, Chuo kimeendelea kutoa huduma kwa wadau wake wote.



Kwa hiyo ni wazi kwamba siku ya uchaguzi, yaani tarehe 31 Oktoba 2010, vituo vya kupigia kura vilivyopo ndani ya kampasi za Chuo Kikuu cha Dar es Salaam vitawapokea na kuwahudumia watu wote wenye stahili ya kupiga kura hapo bila usumbufu wowote. Watakaohudumiwa kwa mujibu wa taratibu zilizowekwa na Tume ya Uchaguzi ni pamoja na wanafunzi, wafanyakazi waliojiandikisha Chuoni na wananchi kutoka maeneo yanayozunguka kampasi za Chuo.



IMETOLEWA NA OFISI YA UHUSIANO

CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM









from: http://www.wavuti.com/4/post/2010/10/ufafanuzi-kuhusu-wanafunzi-udsm-kupiga-kura-2010.html?utm_source=feedburner&utm_medium=email&utm_campaign=Feed%3A+wavuti+%28Wavuti%29&utm_content=Yahoo%21+Mail#ixzz12mrAfLvR

No comments: