Pages

Wednesday, October 20, 2010

Tunduma mwendelezo

Habari zilizozagaa kwenye tovuti mbalimbali ya kuwa TRA wamekamata shehena ya mfanya biashara maarufu wa kampuni ya AZAM Bw. Said Bakhresa, kuwa lori lake lilisheheni karatasi za wapigakura ya URAISI ambazo tayari zimekwisha kupigwa "NDIYO" kwenye picha ya Raisi anayetarajiwa kubwaga manyanga baada ya uchaguzi huu, Bw. JK zimeleta hisia kali miongoni mwa wapigakura kuwa hakuna namna CCM inaweza kufanya hujuma hii ya kuwadhulumu wapigakura bila ya kuwa imepata mwanya kutoka kwa NEC.




NEC hivi sasa ambayo wajumbe wake wote ni teule ya Jk hakuna mpigakura anayeiamini hata chembe kutokana na maamuzi yafuatayo ambayo imeyafanya:-



1) Kufuta haki ya wapigakura kuwa mita 200 kutoka kwenye vituo vyao vya kupiga kura. Hii inaashiria ya kuwa NEC wapo beneti na CCM katika kuhakikisha ya kuwa kura bandia zinapoingizwa kwenye vituo vya kupiga kura wapigakura hawatakuwepo kuzuia au kukamata ushahidi wa uovu huo.



2) Kuanzisha matumizi ya tekinolojia nyingi na ambazo ni rahisi kurubuniwa na mitambo ambayo si rasmi na hivyo kufanya uwepo uwezekano mkubwa wa kucheza na kuyachakachua matokeo halisi ya uchaguzi huu.



3) NEC kutowapigania wapigakura wa vyuo vikuu wapatao 60, 000 na kuanza kutupiana mpira na serikali ya CCM ikithibitisha zaidi wanajua wanachokifanya hapo. NEC wangeliweza kabisa kuahirisha uchaguzi kwa wiki moja ili wanafunzi hao wapate haki yao ya kupiga kura lakini kamwe NEC haitafnya hivyo kwa sababu lengo ni kupunguza kura za upinzani



4) NEC siyo mgeni katika kucheza rafu. Mwaka 1995, ilichelewesha vifaa vya kupiga kura Mkoa mzima wa Dar-Es-Salaam ili kuilinda CCM iliyokuwa inadondoshwa vibaya hapo. Kama wapo tayari kufanza hivyo siku hizo ni lipi la kuwazuia safari hii kucheza rafu tena za kisomi zaidi?



5) Hadi sasa NEC haijatoa tamko rasmi la kupinga au kukubali kuwa chaguzi hii tayari imeingiwa na dosari ya kura za JK kujaribu kuingizwa kinyemela huko Tunduma na mfanya biashara wa kiarabu Bw. Bakhresa na kampuni yake ya AZAM kuingiza kura haramu hizo. Hili linaongeza mashaka ya kuwa NEC ni sehemu ya mkakati huo ndiyo maana imekaa kimya.



6) NEC ndiyo waliochapisha kura hizo sasa inakuwaje JK na watu wake wajue NEMBO hizo kama siyo NEC hao hao waliovujisha NEMBO hizo? NEC walidai wameikodisha kampuni kutoka UK ili ifanye kazi ya kuchapisha kura kuondoa malalamiko kama yaliyojitokea sasa yawaje Afrika kusini wameweza kuziiba nembo hizo na kuzichapisha. KAMA UFEDHULI HUU NI WA KWELI BASI NEC inabidi iwajibike na kujiuzulu ili kuleta imani kwa wapigakura na chaguzi ikaahairishwa na tukajipanga upya



7) Kutokana na ukimya wa NEC wa kuvuja kwa NEMBO zake za uchaguzi na wao kukaa kimya wapigakura wana kila sababu ya kuutilia mashaka uchaguzi huu kama utakuwa ni huru na wa haki. NEC walipaswa kutoa tamko kama ni la kukiri basi kutoa tenda nyingine ya kuzuia NEMBO zilizoibiwa kutumika tena katika uchaguzi huu....



8) Tamko la JWTZ la kuwatisha wapigakura kutoleta fujo baada ya matokeo kutangazwa liliashiria ya kuwa CCM yaelewa kuwa wapigakura hawataafiki matokeo yatayotangazwa na NEC kwa sababu watakuwa wameiba kura kimacho macho na kuzima tafurani hiyo ni kulitumia JWTZ na vitisho vyake.

No comments: