Pages

Wednesday, October 20, 2010

Uvumi wa kukamatwa kwa karatasi za kupigia kura Tunduma

Uvumi wa kukamatwa kwa karatasi za kupigia kura Tunduma


Taarifa kutoka Tunduma, mpakani mwa Tanzania na Zambia mkoani Mbeya zinasema kuwa lori la kampuni ya Azam linalomilikiwa na mfanyabiasha maarufu Bakhresa leo hii tarehe 18 Oktoba, 2010, limekamatwa likiwa na shehena kubwa la karatasi za kupigia kura zitakazotumika uchaguzi mkuu Oktoba 31.



Maafisa wa TRA tunduma walishtuka baada ya kukuta karatasi hizo za kupigia kura zimefichwa kwenye shehena ya vipodozi. Inasemekana kuwa mzigo huo wa karatasi za kupiga kura ulitokea Afrika Kusini na ulipakiwa kwenye gari la Azam kutoka kwenye gari lililotoka na mzigo kutoka Afrika Kusini.



Taarifa zinasema kuwa lori hilo la Azam linashikiliwa na TRA na mzigo huo umekuwa sealed. Kuna hofu kuwa vigogo wenye njama za kuiba kura wanaweza kujaribu kufuta ushahidi kuhusu kukamatwa kwa karatasi hizi za kupiga kura.



Kwa mujibu wa taarifa hizo, karatasi hizo za kupiga kura tayari zimewekewa tiki kumchagua Jakaya Kikwete wa CCM na lengo ni kuwa zisambazwe kwenye vituo mbalimbali vya kupigia kura nchini na zihesabiwe kama kura halali.



Taarifa zaidi zinadai kuwa polisi wanaendelea na uchunguzi

No comments: