Pages

Tuesday, April 13, 2010

TCU na njia mpya ya udahili vyuoni

Natanguliza pongezi zangu kwa TCU kwa utaratibu huu mpya wa udahili vyuoni. hii itarahisisha kupunguza udanganyifu wa vyeti. lakini TCU wanatakiwa kuwahakikishia watoto wa wakulima ambao mara nyingi makazi yao ni vijijini watadahiliwa vipi wakati hawana simu na pia inawezekana hata wazazi wao hawana simu? pia kuna swala la upatikanaji wa network, sehemu nyingine network hakuna mfano morogoro vijijini eneo la kibungo juu bado simu nyingi hazipati mtandao. najua zipo changamoto nyingi hivyo wadau wa elimu hatuna budi kuziangalia na kuja na mikakati ya jinsi ya kutatua changamoto hizo. pamoja na changamoto hizo ninaomba niseme huo ni mwanzo mzuri na hongereni TCU

No comments: